Print

Lugha yoyote ila hukua na kuenea au kudidimia kutengemea mikakati juhudi na ushirikiano wa wadau wote.  Ili kuimarisha lugha sharti washika dau wote;  hususan wasomi wajitoe mhanga kuitetea na kuichangia na kuhimiza wazungumazaji wake juu ya umuhimu wa kuimarisha.

Baada ya uhuru wakenya wengi waliurithi mfumo uliokitweza Kiswahili na kukikuza kiingereza. Baadhi ya wakenya katika maoni yao walisema Kiswahili kilifaa sana sio tu kama chombo cha kuleta umoja wa kitaifa bali pia chombo cha mawasiliano katika Afrika mashariki na kati.
Tume nyingi zilizoundwa zilipendekeza Kiswahili kiwe somo la lazima katika shule za msingi humu nchini.  Jambo hili ni la kutiliwa maanani kwa sababu ndiyo mwanzo wa mtazamo mpya kuhusu Kiswahili.

Wanenaji wa lugha hii upata fursa ya kuifurahia bahari kubwa ya Kiswahili na kuwasiliana kwa ufasaha. Kunazo stadi kadhaa za Kiswahili tukiangazia kukifundisha *mathalan kusoma kuongea na kuandika. 

Lugha ya Kiswahili ina utajiri mwingi wa visawe, methali msamiati, semi tashbihi, tanakali za sauti na fani nyingi ambazo humfanya mtumiaji wa lugha hii kuona fahari kutumia.
Wanafunzi wanapaswa kuhimizwa kukienzi na kuonekana wa kifurahia kuongea lugha hii ambayo ikiwa unaikubali kama lugha ya taifa na kutumiwa ofisini.

Kuanzia madarasa ya chini ambayo ni darasa la kwanza, darasa la pili na tatu,  wanafunzi wahimizwe kuwa msingi watakaojenga hapo ndio utakao baini kama nyumba yao ya lugha ya Kiswahili itakuwa imara au kuyumba yumba.
Walimu pia nao wawe ni wenye heri na furaha tele wanapopatiwa somo la Kiswahili kufundisha katika madarasa hayo katika upande huu natilia mkaza nikirejelea jarida lililotangulia ambapo lilizungumzia uajibikaji wa wazazi katika kuimarisha lugha hii.
Mwalimu wa kufunza Kiswahili katika madarasa ya chini awe ni mwenye mapenzi ya dhati ya  Kiswahili, asiwe ni kukifunza tu kwa maana amepelekwa darasani.  Mtoto akiwa na umri huo ndio wakati mwafaka  wa kujenga lugha yoyote mwalimu anayotaka.

Hivyo basi ni jukumu la sisi zote kushirikiana maana twaelewa kuwa umoja ni nguvu.  Wakati umekwisha wa kunyoosheana vidole na kushika jembe mpini na kwenda kazini.

Changamoto kwetu sisi sote tutarajia wakati mmoja kupita Kiswahili lugha unayotazama kama rahisi ikifanywa ujana katika mtihani wa taifa.  Mwanzo wa kuimarisha lugha hii ni kuelewa umuhimu wake.  Tusichoke sisi walimu na washika dau wengine tuwe wa kwanza kukitumia Kiswahili kwa maana mwana au mtoto hutazama kisogo cha nina.